Song of Solomon 3


1 aUsiku kucha kwenye kitanda changu
nilimtafuta yule moyo wangu umpendaye;
nilimtafuta, lakini sikumpata.

2 Sasa nitaondoka na kuzunguka mjini,
katika barabara zake na viwanja;
nitamtafuta yule moyo wangu umpendaye.
Kwa hiyo nilimtafuta lakini sikumpata.

3 bWalinzi walinikuta
walipokuwa wakizunguka mji.
Nikawauliza, “Je, mmemwona
yule moyo wangu umpendaye?”

4 cKitambo kidogo tu baada ya kuwapita
nilimpata yule moyo wangu umpendaye.
Nilimshika na sikumwachia aende
mpaka nilipomleta katika nyumba ya mama yangu,
katika chumba cha yule aliyenichukua mimba.

5 dBinti za Yerusalemu, ninawaagiza
kwa paa na kwa ayala wa shambani:
Msichochee wala kuamsha mapenzi
hata yatakapotaka yenyewe.

Shairi La Tatu

Mpenzi


6 eNi nani huyu anayekuja kutoka jangwani
kama nguzo ya moshi,
anayenukia manemane na uvumba
iliyotengenezwa kwa vikolezo vyote
vya mfanyabiashara?

7 fTazama! Ni gari la Sulemani
lisindikizwalo na mashujaa sitini,
walio wakuu sana wa Israeli,

8 gwote wamevaa panga,
wote wazoefu katika vita,
kila mmoja na upanga wake pajani,
wamejiandaa kwa ajili ya hofu za usiku.

9 Mfalme Sulemani alijitengenezea gari;
alilitengeneza kwa mbao kutoka Lebanoni.

10 hNguzo zake alizitengeneza kwa fedha,
kitako chake kwa dhahabu.
Kiti chake kilipambwa kwa zambarau,
gari lake likanakshiwa njumu kwa upendo
na binti za Yerusalemu.

11 iTokeni nje, ninyi binti za Sayuni,
mkamtazame Mfalme Sulemani akiwa amevaa taji,
taji ambalo mama yake alimvika
siku ya arusi yake,
siku ambayo moyo wake ulishangilia.
Copyright information for SwhKC